-->

Type something and hit enter

By On
Wanawake wa Kijiji cha Katisunga wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi wamehofia ndoa zao kuvunjika kutokana na makundi ya wasichana wadogowadogo kuvamia Kijiji hicho na kufanya biashara ya ngono kwa bei chee ya shilingi 1000, huku wakipewa majina ya panya road na damu chafu.

Wasichana hao ambao kwa umri wanadaiwa kuwa ni wadogo wanatoka katika maeneo tofauti tofauti ya mkoa wa Katavi ambapo kila siku majira ya saa 1:00 jioni huanza biashara hiyo wanayoifanya hovyo hadi kwenye milango ya watu inayosababisha kero kwa baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho.

Wakazi wa Kijiji hicho wameliomba Jeshi la Polisi kufanya msako mkali na kuwakamata wasichana hao ambao wanafanya biashara ya ngono hadharani kwa kulinda maadili ya watoto wanaoendelea kukua wasiharibikiwe.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Ali Makame, akizungumza kwa njia ya simu amekemea vitendo hivyo na kuwataka wazazi kuwalea watoto katika maadili, kuwapeleka shule, kuwapa huduma za msingi huku akisisitiza kuwakamata watoto wote wanaofanya biashara hiyo.

Weka maoni yako hapa