Kufuatia uwepo wa tetesi za muda mrefu kuhusiana na kipa Farouk Shikalo anayekipiga katika klabu ya Ndari FC kutua Yanga, hatimaye uongozi wa timu hiyo umekanusha taarifa hizo. Imeelezwa.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Kenya zinasema kuwa mabosi wa Bandari wameitaka Yanga kumsahau kipa huyo kwani bado ana mkataba wa miaka miwili.
Mabosi hao wamesema hawataweza kumuachia Shikalo sababu ana mkataba na bado wanategemea huduma yake.
Tetesi za Shikalo kutua Yanga zimechukua takribani nusu msimu sasa tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara lakini imekuwa ngumu kupata saini yake.
Mpaka sasa Yanga imekuwa ikitegemea zaidi huduma ya makipa wake wawili Ramadhan Kabwili na Klaus Kindoki.